Nani Atazungumza kwa Niaba yao?
“Watoto wa sikuhzi
hawana adabu,hawaheshimu wakubwa,wanaongea lugha chafu,hawavai mavazi ya
heshima,wala hawafanyi vizuri katika kazi wanazoepewa”. Hii ilikua sauti ya mwanamke akilalamika kuhusu kizazi
kilichozaliwa mwaka 1990 na kuendelea.
Labda yupo sahihi, au Labda hayupo sahihi, simhukumu, lakini
sentensi yake ilinikumbusha kuhusu neno moja Garbage in-Garbage out, kwenye komputa na Nyanja nyingine,
linatumika kueleze wazo kwamba ukiweka kitu kibovu au chenye thamani hafifu
utapata matokeo mabovu.
Kabla hatujalalamika kuhusu namna wanaishi tuanglie
nini tunawapa. Kwanza watoto wanakua kwenye mazingira ya kelele(miziki, matusi,
na televisheni). Na hata kwa sasa maeneo ya vijijini ambapo familia zinaweza
kukosa hata radio, watoto wanasikia fujo hizo kwenye pikipiki (bodaboda) ambao
wanipiga miziki hiyo kwa uhuru barabarani. Watoto hawa wanachukua yote, na
kutoka na umri wao, hawajui kipi bora kwao, hawajui ni mavazi gani wavae,
miziki gani wasikilize, magazeti au majarida au vitabu gani wasome, wala
hawajui ni kipindi gani cha kuangalia kwenye televishion. Wanakua katika
mazingira ambayo wazazi wako shughulini na walimu pia, hakuna mtu anachukua
jukumu la kuwapa taarifa sahihi. Siku
moja nilisikia mzazi mmoja anasema “Nafurahi mwanangu ana miaka 5 sasa
ninampeleka kwa walimu wamfundhishe adabu” wakati huohuo walimu
wanalalamika wanafunzi hawana adabu ni tunaacha mzigo kwa wazazi wao.Wazazi
wanatumia muda mwingi katika kazi na biashara ndogondogo, ambalo ni jambo jema,
lakini hawapati hata muda wa saa moja kuongea na watoto wao au hata
kuwafundisha maadili.
Kama hali ipo hivi, tunategemea nini kuhusu tabia zao?
Watatoa wanachopokea. Tunalalamika kuhusu
tabia ya kizazi kipya bila kuangalia kwa makini kitu kitu gani
kimewafanya wawe hivyo. Kizazi hiki hakina tatizo lolote, ila wanatoa kile
wanachopokea, huwezi kupanda mti wa limao ukategemea tikitimaji litakua hapo.
Wazazi, Walimu na Majirahi ni wajibu wetu sote
kuchukua jukumu la kuhakikisha kizazi hiki kinapata taarifa sahihi ili wawe
raia wema baadae.
Imeandikwa: 2 Machi 2018, Gloria Busungu
Maada : Familia, Marafiki, na Jamii
Comments
Post a Comment