Nani Atazungumza kwa Niaba yao?
“Watoto wa sikuhzi hawana adabu,hawaheshimu wakubwa,wanaongea lugha chafu,hawavai mavazi ya heshima,wala hawafanyi vizuri katika kazi wanazoepewa”. Hii ilikua sauti ya mwanamke akilalamika kuhusu kizazi kilichozaliwa mwaka 1990 na kuendelea. Labda yupo sahihi, au Labda hayupo sahihi, simhukumu, lakini sentensi yake ilinikumbusha kuhusu neno moja Garbage in-Garbage out , kwenye komputa na Nyanja nyingine, linatumika kueleze wazo kwamba ukiweka kitu kibovu au chenye thamani hafifu utapata matokeo mabovu. Kabla hatujalalamika kuhusu namna wanaishi tuanglie nini tunawapa. Kwanza watoto wanakua kwenye mazingira ya kelele(miziki, matusi, na televisheni). Na hata kwa sasa maeneo ya vijijini ambapo familia zinaweza kukosa hata radio, watoto wanasikia fujo hizo kwenye pikipiki (bodaboda) ambao wanipiga miziki hiyo kwa uhuru barabarani. Watoto hawa wanachukua yote, na kutoka na umri wao, hawajui kipi bora kwao, hawajui ni mavazi gani wavae, miziki gani wasikilize, magazeti au majarida au